Listen

Description

Je, lugha unayozungumza ndiyo kitambulisho chako? 🎙️

Katika Bongo Bila Borders Episode 13 tunaizungumzia lugha kama pumzi ya utambulisho, kama mwanga unaoangaza njia mpya, na kama mlango unaoweza kufunguka unapozungumza zaidi ya lugha moja. Tunagusia namna maneno yanavyoweza kukuinua, kukutambulisha na kukupa nafasi ambazo wengine hawazifikii kwa urahisi. Lugha ni nguo tunazovaa, ni muziki tunaoubeba, na ni pasipoti ya roho katika safari yetu ya dunia.

Tunalisheheni pia penzi la Kiswahili, lugha inayokua kwa kasi na kuufikia ulimwengu kwa sauti ya ujasiri. Leo linasikika kwenye utafiti, kesho kwenye biashara, keshokutwa kwenye sanaa na diplomasia. Wimbi lake linapanuka na kuunganisha tamaduni nyingi kama mkondo wa maji unaokutana na bahari. Huu ni wakati wa kuikumbatia lugha yetu kwa fahari, kuiendeleza kwa bidii na kuiruhusu iitupe mbali kadiri upepo wa dunia unavyovuma. ✨

Karibu usikilize, ujisikie na utafakari nasi, kwani lugha hasa Kiswahili lina uwezo wa kutuunganisha, kututia nguvu na kutupa nafasi ya kuona dunia kwa macho mapya na moyo ulio wazi.