Listen

Description

Wanaume hawajui namna ya bora ya kuwasiliana, kuanzisha mazungumzo ya muhimu na inawezekana hawajui kabisa kuongelea wanayoyapitia, wanayoyafikiria au kuelezea hisia zao wakiwa kwenye mahusiano, hii ni dhana iliyojengeka kwa watu wengi sana, je ina ukweli wowote?

Baadhi ya wanaume wanapingana na hili, na wanasema si kweli. Wanaume wanaweza sana kuwasiliana, sema tu wanawasiliana kwa namna ambayo ni tofauti na inahitaji muda kuielewa.

Michael na Nadia wanazungumza kwa kirefu sana na Gillsant pamoja na Leslie juu ya mawasiliano, matarajio na changamoto za kutokuwa na mawasiliano mazuri kwenye mahusiano kwa upande wa mwanaume na namna gani mawasiliano yanaweza kujenga au kubomoa kabisa mahusiano hayo.