Listen

Description

Sadick Ali ni mchekeshaji, muigizaji, mfanyabiashara... na zaidi ya yote—ni baba. Sasa, kama wanaume wengi duniani, wazo la kuwa baba kwa mara ya kwanza lilimjia kama mshangao wa mitihani ya darasa la saba: hauko tayari, lakini unajidanganya kuwa utaweza!

Na kama ulivyotegemea, Sadick alijikuta akikabiliana na mchanganyiko wa hisia—uoga, shauku, na sintofahamu isiyokuwa na GPS. Lakini kubwa zaidi, aligundua ukweli mchungu: hata uki-google kila kitu, hakuna njia ya kujiandaa kikamilifu kwa "daddy duties." Na ukifikiri unajua, mtoto wako atakutengenezea changamoto mpya—au diapers zitakutengenezea!

Karibu katika Men Men Men The Podcast, ambapo Michael, Sadick, na Nadia wanazama kwa kina (na kwa vicheko) kwenye changamoto na baraka za kuwa baba kwa mara ya kwanza. Hii ni safari inayochanganya furaha, machungu, na maswali kama: “Mbona mtoto hajalala bado?”