Listen

Description

VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
_By Luphurise Mawere_

*14. Fanya Kazi kwa Bidii na kwa Werevu*

_2 Timotheo 2: 6-7_
_6 Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda._

_7 Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote._

Mithali 22: 29

_Mithali 16: 3 Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika._

Unaposoma hiyo mistari hapo juu utaona tunatakiwa kufanya kwa bidii ndio lakini kwa *werevu* pia. Kwa Kiingereza wanasema _Work Hard and Smart_
Wengi wameishia kufanya kazi kwa bidii tu huku wakijichosha, wakisota yaani *kutoil*, hawapumziki, hawalali kiasi kwamba hata muda wa kufurahia matunda ya walichokisotea hawana.

*Kufanya kazi kwa bidii tu au kusota ni nini?*
Ni kuzitegemea akili zako, elimu yako, biashara zako, kazi zako kutegemea nguvu zako ukifikiri ndivyo vitakuletea mafanikio.
Wengi wamekuwa busy kukimbizana na fursa kubwa na za kimataifa, kuongeza elimu kubwa, kufanya biashara kubwa zinazowafanya kusota masaa mengi, wengine hata hawaonekani, wengi wanaondoka nyumbani saa 10 wanarudi saa 4 za usiku hata watoto na familia yako haikuoni.

Wengi hawana hata muda na Mungu wakikimbiza mafanikio kwa akili zao

Siko kinyume na kupata elimu kubwa , biashara na kazi za kimataifa, vitu vikubwa hapana ila vifanyike kwa werevu

*Kuwa mwerevu ni nini?*
_Mithali 3: 5-6_
Kuwa *Mwerevu* ni KUMTUMAINI Bwana kwa moyo wako wote, kutokuzitegemea akili zako mwenyewe, kumkiri Mungu katika njia zako zote, ili anyooshe mapito yako.

_Mwanzo 41: 15-16, 41_
Ukiangalia namna Yusufu alivyofanikiwa Misri ambapo alikuwa mtumwa tena alikuwa mfungwa ndio utaelewa maana ya kuwa *Mwerevu*.
Humuoni Yusufu *akitoil* huoni akisota, huoni akijichosha ila alikuwa mwerevu alijua namna ya kufanya vitu sahihi ambavyo vitampa mafanikio.
Yusufu *aliweka tumaini lako lote kwa Bwana* maana unaona Farao anapomuuliza swali kwamba nasikia unajua kutafsiri ndoto Yusufu anajibu _mstari wa 16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani._.
Umeuona werevu mpendwa wangu?
Ni kutambua kuwa wewe huna kitu chochote ambacho kinaweza kukufanikisha bali yuko Mungu amilikiye vyote na yeye ndio anayetubariki watoto wake
Kukubali kunyenyekea na kuongozwa na Mungu katika njia zako zote
Na unaona Yusufu alipomkabidhi Mungu anapata nguvu na upako wa kufsiri ile ndoto sawasawa kabisa na hii inampa kibali kwa Farao na anawekwa kuwa Waziri Mkuu wa Misri.
Mpendwa wakati wa kusota umeisha
Wakati wa kukesha bila matunda umeishs
Wakati wa kujitaabisha umeisha
Hebu tafakari tangia ulipoanza kujichosha, kujitaabisha, kukosa hata muda na familia na Mungu Je umeshapata hayo mafanikio?
*Sasa ni wakati wa kubadilisha strategy*
Kutambua kwamba Bwana asipoijenga nyumba wajengao wafanya kazi bure ( _Zaburi127:1_)

Mungu akuwezeshe uweze kufanya kazi sio kwa bidii tu bali kwa werevu

Mawasiliano +255 754 934693