Listen

Description

VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
_By Luphurise Mawere_

*15. Usidhulumu Mali ya Mtu*

*Kumbukumbu la Torati 24: 14-15*
_14 Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako;_

_15 mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako._

*Yakobo 5:4* _Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi._

Watu wengi wanapenda kupata mafanikio ya kiuchumi ila changamoto inakuja kuna mambo hawafanyi sawasawa.
Wengine wanafikiri kwa kuwadhulumu watu hasa masikini na wahitaji ndio watafanikiwa.
Na bahati mbaya tuna watu wa namna hiyo kwenye jamii ambao wanadhani pesa zao zitajaa wakizuia ujira wa wajakazi wao.
Unaweza kusema aah mimi sijawahi kudhulumu hili neno sio langu, please stay with me, endelea kusoma na kusikiliza.

Mpendwa hebu tafakari hili *Je ni wajakazi wangapi, vibarua, mafundi, wataalamu, wafanyakazi wako n.k. wangapi ambao walikufanyia kazi na hukuwalipa kwasababu moja au nyingine?*

Kinachosikitisha ni kwamba mara nyingine watu ambao tunawaona wamefanikiwa, wenye makampuni makubwa, biashara kubwa na kazi kubwa ndio wamekuwa mstari wa mbele kudhulumu wajakazi wao.
Tena wengine wanasubiri karibu na tarehe za mshahara au za kulipa ndio wanawaambia wajakazi ooh hufanyi kazi vizuri, kumbe wanafanya hivyo ili wasilipe msharaha.
Mpendwa dhuluma ni chukizo mbele za Mungu

*Mambo matatu (3) ya kujifunza;*
▪Kuwalipa wajakazi na watu wote wanaotufanyia kazi kwa wakati, usiwazungushe, usimwambie baadae wakati una uwezo wa kumpa muda huo. Kama huna mwambie muda wa uhakika wa kumpa nae aridhie. Kinyume na hapo usilale la ujira wao, Kuwa mtu wa haki
▪Watu hawa wanaokufanyia kazi wengine ni maskini na wahitaji, wanautumainia huo ujira waendeshe maisha yao. Wana familia na watu wanaowategemea kama wewe
Wale wenye wasaidizi wa kazi unamwambia nakuwekea pesa halafu ikifika siku ya kumlipa unaanza kumkata pesa hiyo ni dhuluma mpendwa
Jiweke kwenye viatu vyao
Je wewe ungependa kufanyiwa kama wao?
▪Ukifanya hila na kuzuia ujira wa hao watu kwa kuwadhulumu, wakampigia Mungu kelele kwa vilio na Mungu atasikia na hii itakuwa ni dhambi kwako.
Lakini _Wagalatia 6:7b inasema chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna_
Mpendwa panda mema, panda haki usipande dhuluma kama unataka mafanikio ya kiuchumi
Usipende kufaidikia mgongoni mwa watu wanyonge au ambao unajua hawawezi kukufanyia kitu.
Mungu akuwezeshe uishi maisha ya kutenda haki. Uwe na Juma lenye Ushindi

Mawasiliano;
*+255 754 934693*