2 Wafalme 4: 1-7
Hesabu 27: 1-11
_Nehemia 2: 20 Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu._
Mistari hiyo hapo juu inaonyesha namna ambavyo Mwanamke mjane na mabinti za Selofehadi walikuwa kwenye changamoto kubwa. Walikuwa kwenye mazingira ambayo kibinadamu yalikuwa hayawezekani
Mama mjane alikuwa na madeni na watoto wake wawili walikuwa wachukuliwe kuwa watumwa ili kulipia deni aliloacha baba yao ambaye alikuwa amekufa.
Huyu mama alikuwa kwenye financial crisis na kibinadamu alikuwa hana kitu chochote cha kumsaidia kulipa yale madeni. Alipokwenda kwa mtumishi wa Mungu Elisha anaambiwa akaombe vyombo vya mafuta tena asitake vichache.
Mwanamke mjane anaamini Mungu atamfanikisha na kutii maelekezo aliyopewa na mtumishi Elisha na kwa kufanya hivyo Mungu anakomesha changamoto yake, ghafla nyumba yake inageuka kuwa kiwanda cha mafuta anapata pesa analipa deni na kupata fedha za kutumia na watoto wake.
Mabinti za Selofehadic halikadhalika waliamini wakienda kwa Mungu atawapa urithi wao na hakika kwa Imani yao walipata urithi na sio wao tu ombi lao likageuzwa kuwa haki na hukumu Israeli kwamba Wanawake wataruhusiwa kurirhi kama mtu hana mtoto wa kiume.
Nehemia alipoamua kuujenga uliokuwa umeharibiwa wa Yerusalemu alipata upinzani mkubwa kutoka kwa maadui zake kina Sanbalati, Tobia na Geshemu mwarabu. Maadui zake hao walimcheka na kumdharau lakini Nehemia anawaambia Mungu wake atawafanikisha na hakika Ukuta ule unakamilika ndani ya siku 52.
Mpendwa unapitia jambo gani?
Yamkini mume ameondoka, ndoa imekufa kabisa
Inawezekana unapitia pagumu umejifungia ndani kwa kukata tamaa
Au una ugonjwa ambao umeambiwa hauna tiba, au ni kansa wamekuambia imefika stage ambayo huwezi kupona
Mpendwa ninakuletea Mungu anayeweza yote siku hii ya leo
Mungu asiyeshindwa na chochote
Ili Mungu aingilie kati hiyo yali yako unapaswa kumwamini maana pasipo Imani hatuwezi kumpendeza Mungu.
_Waebrania 11: 1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana._
Mpendwa usiangalie mazingira yanasemaje, mwanamke mjane hakuangalia majirani na marafiki zake watasema nini anavyoomba vyombo. Wala Mabinti za Selofehadi hawakuangalia wataonekanaje maana walikuwa wanaomba kitu kilicho kinyume na taratibu za taifa lao la Israeli. Lakini Wanawake hawa wote walijua kitu kimoja yuko Mungu, NIKO AMBAYE NIKO yeye atawafanikisha. Basi!
Kuna mahali inabidi ufike usiangalie ripoti ya madaktari inasemaje, taratibu za ukoo zinasemaje, mazingira yanasemaje bali unamwangalia Mungu kwamba Mungu ni kweli nimefika miaka 40 lakini ninajua nitaolewa na nitapata mtoto.
Ni kweli Mungu sina hela na sijalipia watoto wangu ada ila najua wataenda shule maana kuna namna utafanya ambayo mimi sijui ni namna gani.
Yaani kuna saa inabidi uende mbele za Mungu kama kichaa na Crazy Faith
Unaamini vitu kama mjinga hapo ndipo utamuona Mungu
Imani ndio Currency yaani fedha ya kimbingu ya kupata vitu vya Mungu
Vitu vya Mungu haviitaji Logic, ukiweka logic unamiss point na watu wengi tumekosa miujiza yetu kwasababu ya kutumia logic.
Mpendwa yakupasa kujua kwamba Mungu tunamtumikia sio sawa na wewe au mwanadamu yoyote, Mungu ni Mungu mkuu yeye ndio ameumba kila kitu na kila kitu ni chake na ANAWEZA KUFANYA mambo YALIYOSHINDIKANA
Amini tu!
Uwe na Juma lenye ushindi
Kusikiliza masomo yote yaliyopita bonyeza link hii hapa
*Mawasiliano*
+255 754 934693