Listen

Description

VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
_By Luphurise Mawere_

*7. Kuijaza Nchi*
_Mwanzo 1: 28_

_Ezekiel 27: 25 Merikebu za Tarshishi zilikuwa misafara yako, kwa bidhaa yako; nawe ulijazwa sana, ukawa mtukufu sana, katika moyo wa bahari._

_Isaya 23: 2_
Mungu mojawapo ya kazi waliyopewa Adam na Eva ni kuijaza nchi. Mungu anataka mimi na wewe tuijaze nchi baada ya kuzalisha na kuongezeka
Hiyo bidhaa ambayo umeizalisha inapatikana wapi?
Umeijaza wapi?
Au bidhaa zako zinapatikana kwa ndugu zako tu na watu wa mtaani kwako tu?
Kama unataka kufanikiwa kiuchumi itakupasa uijaze Dar es Salaam, Tanzania, Afrika na ulimwengu wote na vipaji, karama, ujuzi na bidhaa zako
Unaanza kidogo lakini lengo liwe kubwa la kuijaza nchi na kile Mungu alichokubarikia nacho
Nyimbo unazoimba zisiishie kanisani kwako tu au mkoani kwako tu na nchini kwako tu, ijaze nchi mataifa wamsikie Mungu wako kwa nyimbo zako
Unaweza kuwa wa Kimataifa bila kujali mazingira
Kuna dada anaitwa Mphumi ni mzaliwa wa Africa ya Kusini, alikuwa chokoraa lakini leo ni Mhamasishaji wa Kimataifa anajaza mataifa maarifa ya kumaliza tatizo la watoto wa mitaani na amesaidia wengi wakarudi shule.
Mwimbaji wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Sinach haikuwa rahisi kwake kuanza uimbaji maana baba yake hakumkubalia , lakini leo ulimwengu umejaa nyimbo za Sinach zikiwatia watu moyo na kuwasogeza kwa Mungu wao
Angeangalia mazingira tusingekuwa tunasikia nyimbo zake leo
Je huko kwenye mitandao ya kijamii unafanya nini? Unaangalia maisha ya watu au uko busy kuijaza na kile Mungu alichokubariki nacho
Chukua maamuzi sahihi sasa, amua kuijaza nchi na kile Mungu alichokupa
Ulimwengu unasubiri udhihirisho wako
Kuna watu wamekwama kwasababu ulichonacho hakijawafikia, Jaza nchi.

Uwe na Juma lenye baraka na ushindi tele

_*Masomo yaliyopita yote yanapatikana katika link hii WATUMIE WATU WENGINE WAJIFUNZE*_

+255 754 934693