Wagalatia 6: 7-9_
_6 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna._
_8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele._
_9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho._
_2 Wakoritho 9: 6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu_
Mpendwa umepanda nini kwenye maisha ya watu?
Unavuna nini kwenye maisha yako?
Matunda ambayo umeyapata kwenye maisha yako yanatokana na vitu gani ulivyovipanda? Vitu vyema au vibaya?
Je umevuna mambo uzima wa milele au umevuna uharibifu?
Au umevuna haba au umevuna ukarimu?
Watu wengi wanatamani kuvuna matunda mema kwenye maisha yao, leo neno limekuja kutukumbusha kuwa mavuno tunayoyataka yanategemeana na vitu tulivyopanda.
Kama umepanda mema utavuna mema, kama umepanda uharibifu utavuna uharibifu.
Ukipanda Bamia, Usitegemee kuvuna Strawberry
Ukipanda nyanya usitegemee kuvuna apples
Kama utataka kuvuna apple itabidi upande apple
Hivyohivyo kama umepanda hila, chuki, fitina kwenye maisha ya utavuna uharibifu tu siku moja
Kama uko kwenye ajira ukapanda fitina kwenye maisha ya watu ili wewe upendwe na bosi ili upandishwe cheo au kuongezewa mshahara basi nikukahikikishie kwamba utavuna tu hilo pando ulilolipanda.
Kama ni mtoto umepanda kutotii wazazi wako lazima utavuna tu, na watu wataona tu maisha yanavyoenda.
Kuna watoto wanatukana wazazi wao, wanawafanyia wazazi vituko vikubwa sana wamekuwa tanzi kwa wazazi wao wengi wameishia pabaya wamevuna uharibifu.
Tunao watu wengi wenye jamii leo ambao wamevuna uharibifu kwasababu ya kushindwa kuheshimu wakubwa.
Miaka yangu ya mwanzo mpaka darasa la 5 nilikulia Kijijini, kule kila baba ni baba yako, kila mama ni mama yako, tulilelewa kuwatii wakubwa wote hata kama hajakuzaa au humjui. Ukiona mtu mkubwa kabeba mzigo utamsaidia hata kama humjui. Nilipokuja Dar es Salaam nilishangaa namna watoto wadogo wanawatukana watu wazima na kuwakosea heshima.
Tena wengine naona vijana wadogo wakiwatukana watumishi wa Mungu kwenye mitandao ya Kijamii, hilo ni pando na watavuna tu uharibifu.
Niongee na Singel Ladies kama uko serious unataka Mungu akupe mume kutoka kwako anza kupanda mema, hayo mahusiano na mume wa mtu acha hilo ni pando na mavuno yake ni uharibifu mkubwa sana. Usitegemee kupata ndoa nzuri wakati kuna mke wa mtu analia mahali kwasababu yako.
Amua leo kupanda mema na hakika utavuna mema.
Niongee na wababa ambao unapanda uharibifu kwa watoto wa watu, unawalawiti na unawabaka yaani utavuna tu uharibifu maana umepanda kwa mwili.
Kama unasoma ujumbe huu na umejikuta mahali umepanda mambo ya mwili ya uharibifu kwenye maisha ya watu na ya kwako, au unapitia kipindi cha mavuno ya uharibifu kwa kile ulichokipanda kwenye maisha ya watu.
Mungu wetu ni mwingi wa Rehema. Ukimlilia kwa toba ya kweli atakusamehe.
Ukihitaji msaada zaidi tuwasiliane
Mungu akuwezeshe Upande mema ili uvune mema wewe na uzao wako
Uwe na Juma lenye Ushindi.
Luphurise Mawere
_Personal Finance & Life Coach_