Listen

Description

VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
_By Luphurise Mawere_

*12. Epuka Kutamani Utajiri wa Haraka*

_Mithali 13: 11 Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa._
Kwa Kiingereza inasema
_Proverbs 13: 11 Wealth quickly got will become less; but he who gets a store by the work of his hands will have it increased._

Tunaishi katika ulimwengu ambao vitu vingi vinafanyika kwa haraka ni maendeleo na kweli vimeturahisishia kazi
Sasa badala ya kupasha chakula dakika 15 unapasha dakika 1
Badala ya kupika masaa 2 unapika dakika 15 tu
Kuna mashine za kufua, kupasi, kufanya usafi na kadhalika
Vitu vinakwenda fasta fasta
Sasa hii imeleta watu wengi kutamani hata mafanikio na Utajiri wapate hivyohivyo harakaharaka
Mtu anamaliza chuo leo anataka hapohapo awe na gari, awe na nyumba au na mapesa kama mtu aliyekaa kazini miaka 10
Mwingine anaanza biashara leo anataka leoleo atengeneze mamilioni
Wana hawataki kabisa kusubiri hawako radhi kuchuma kidogo kidogo
Ukienda kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kumejaa matangazo kibao yenye kuvutia yakitangaza kamari ambapo unaweka kiasi fulani cha pesa halafu unavuna sana
Matangazo mengi ya hizo _Get-rich-quick schemes_ yaani kamari yanayoa ahadi ya kupata pesa mara dufu, nyumba, magari, safari za matanuzi, kwa haraka sana tena bila kufanya kazi yenye tija
Lakini Utajiri wa Kimungu una kanuni zake ambazo nyingi tumezifundisha katika mfululizo huu naomba tafuta uweze kujifunza
Wengi kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka wamepoteza viwanja, majumba, magari, pesa zote, kazi na hata mahusiano na wapendwa wao maana waliwekeza wakidhani watavuna zaidi

Leo Mungu anasema nasi kupitia neno lake naomba usome _Mithali 12: 11_
Mungu anatuasa tuache kukimbizana mambo ya upuuzi, kwa kiingereza inasema _don't chase fantasies_, fanya kazi, lima shamba lako, chuma kidogo kidogo Mungu atakizidisha tu
Tamaa ya Utajiri wa Haraka chukizo kwa Mungu wala haitazaa baraka
_Mithali 20: 21 Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa._

Mungu akusaidie ujiepushe na kutaka mafanikio na Utajiri wa Harakaharaka ufuate kanuni zake za Kufanikiwa naye atakuzidisha, ameaihidi hivyo na atafanya, Amen!

Kupata masomo yote ambayo tumeshafundisha bonyeza hapa

Pia shirikikisha wengine masomo haya