Listen

Description

VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI

_By Luphurise Mawere_

*13. Ishi kwa Mipango*
_Mithali 21: 5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji._

Kiingereza inasema _The plans of the diligent lead only to plenty, but everyone who is hasty comes only to poverty._

Pia soma _Luka 14: 28 - 30_

Je mipango yako ya mwaka huu 2020 ni ipi?
Vitu unavyovufanya viko kwenye mipango yako? Au umekurupuka tu kuvifanya?
Neno hapo juu linasema usipojipanga utauelekea umaskini
Mipango ni muhimu sana maana inakuonyesha wapi unaelekea
Kama hujui wapi unaelekea ina maana utaishia popote
Wengi wamepata hasara, wamepoteza kila kitu na kufilisika kwasababu ya kutokuishi bila mipango
Kabla hujaanza biashara weka mipango
Kama unataka kupandishwa cheo, kuongezewa mshahara au kubadilisha kazi weka mipango kwanza ili usije kufanya makosa
Usikimbilie kuingia kwenye biashara kwasababu wengi wanasema inalipa, ingia kwenye biashara kwasababu iko kwenye mipango yako

Kujipanga kuna faida nyingi kama;
▪Kukupa mwelekeo wa unapotaka kwenda huku ikikupa nafasi ya kuboresha na kurekebisha mipango yako ili usipate hasara
▪Kufanikiwa kwenye mambo yako
▪Kufanya maamuzi sahihi kwenye maisha yako yatakayokuepusha na hasara
▪Inakusaidia kupunguza gharama

Mungu akusaidie uishi maisha yenye mipango

*Kupata mtiririko wa masomo haya bonyeza link hii

Share na wengine waweze kujifunza

Barikiwa sana
+255 754 934693