Listen

Description

Wafilipi 2: 4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

*Ubinafsi* ni ile hali ya kujali mambo yako kwa kiasi kikubwa sana na kuyapa mambo ya wengine nafasi ndogo mno. Kujali mambo yako zaidi na kutoangalia mambo ya wengine kabisa.
Dunia tunayoishi imejaa watu wengi wenye ubinafsi, maendeleo na changamoto zilizoko ulimwenguni zinazidi kufanya watu kuwa wabinafsi. Lakini Mungu wetu hapendi tuwe wabinafsi na ndio maana hili neno limekujia leo.
Hali ya ubinafsi iliyoko duniani inaongezeka sana na imepelekea wengi wenye uhitaji yaani masikini, yatima, wasiojiweza kuongezeka na kukosa msaada kwasababu wale ambao wangesimama kuwasaidia wanaangalia mambo yao zaidi.
Watu wako busy wananakimbizana na kazi na miradi yao kuanzia Jumatatu hadi Jumapili wala kwenye ratiba yake hakuna jambo la mtu mwingine linaweza kuingia. Hali inasikitisha sana maana makanisani ambako wengi walitegemea hali iwe tofauti watu waonyeshe upendo wa Kristo waliombeba nako ubinafsi umetawala. Unakuta mtu anasema ameokoka lakini maombi yake tu ni ubinafsi mtu, ataombea familia yake tu wala hakumbuki wengine hii ni hatari sana. Wengi ukiwashirikisha hitaji la kukuombea watakuambia mpendwa tunakuombea lakini nataka kukuambia kuwa ni wachache sana watakuombea. Ilifika mahali nikamwambia Mungu ninakuomba nisimwahidi mtu nitamuombea halafu nisiweze bora nisiongee na nikimtamkia basi naomba nimuombee kweli.

*Vyanzo vya roho ya Ubinafsi*
▪Malezi mabaya, mara nyingi wazazi tumesababishia watoto wetu kuja kuwa wabinafsi, kuwaonyesha kila kitu walichonacho ni chao na kuwajengea tabia ya kutowapa wenzao vitu vidogo tu kama chakula, michezo n.k
▪Tamaa ya kujilimbilikizia vitu
▪Kujiona bora kuliko wengine yaani wewe tu ndio unastahili kujaliwa na kufanyiwa vitu vizuri

*Madhara ya Ubinafsi*
2 Samueli 11
Yakobo 3: 16
Mwanzo 4: 9
▪Inasababisha mtu aue kama mfalme Daudi alivyomuua Uria kwa ubinafsi wake baada ya kulala na Betshaba mke wa Uria
▪Kuwa muongo mfano Kaini alipomuua ndugu yake Abeli alipoulizwa na Mungu alipo Abeli alisema hajui alipo
▪Ubinafsi unaleta Machafuko na kuwafanya watu watende dhambi

*Namna ya kujiepusha na Ubinafsi*
Wagalatia 2: 20
Marko 12: 31
Yohana 15: 13

▪Inabidi ufe
Yaani utu wako wa kale ufe na umruhusu Kristo ndio aishi. Usulubishwe pamoja na Kristo.
▪Kufuata Amri Kuu inavyosema, Kuwapenda watu wengine kama tunavyojipenda sisi
▪Kujitoa kwa ajili ya wengine bila kutegemea kutendewa sawa na ulivyotenda, jitoe kama sadaka.
Kwenye maisha yanayompendeza Mungu tusienende kama ulimwengu, ulimwengu watatoa kwasababu watatolewa wanasema _scratch my back, I will scratch yours_ huu sio Ukiristo

Wapendwa Yesu Yu Karibu kurudi, tengeneza njia zako
Amua leo kujiepusha na Ubinafsi
Mungu akuwezeshe

0754934693
Luphurise Mawere