Naomba usome pamoja nami *2 Wafalme 7: 3-16*
Watu wengi hawapigi hatua maishani kwasababu ya kukaa sana kwenye mazoea.
Wengi wanatamani kufanikiwa ila hali za kukaa kwenye mazoea zinawazuia kabisa kupiga hatua katika maisha yao.
Mazoea au Comfort zone ni ile hali ya kuwa mahali ambapo panakupa faraja na panakufanya ujisikie amani, usalama na nafuu.
Katika habari tuliyosoma kwenye *2 Wafalme 7: 3-16* tunaona Wakoma wanne huko Samaria ambao ninawaita ma-Champion yaani mashujaa maana waliamua kutoka kwenye mazoea.
Hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana Samaria, kulikuwa na njaa kali na vitu vilikuwa vinauzwa bei kubwa sana.
Hali ilikuwa mbaya mpaka ikafika mahali wanawake wakaanza kula watoto wao.
Ingekuwa sasa tungesema kulikuwa na mdororo wa kiuchumi economic crisis.
Enzi hizo Wakoma walikuwa wanadharauliwa na kutengwa, usingeweza kutarajia chochote chema kutoka kwao.
Wakoma hawa ma-Champion wakaiangalie ile hali wakaona inabidi tu waamue kutoka kwenye mazoea, watoke kwenye comfort zone.
Wanaamua kuchukua hatua
_2 Wafalme 7: 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu._
Waka-Stretch yaani kufanya zaidi, wakasema tukienda mjini kuna njaa hapa kuna njaa na tutakufa, twende kwa adui zetu jeshi la Washami wasipotuua tutaishi wakituua basi tutakufa.
Kwa lugha ya sasa hawa walisema ndugu zangu LIWALE NA LIWE!
Wakatoka kwenye mazoea.
Kumbuka ni Wakoma mpendwa, na wanakoenda ni kwa jeshi na hawana uwezo kabisa wa kupigana na hili jeshi.
Wanafanya maamuzi magumu yanayohatarisha maisha yao.
Ooh ninampenda Mungu wanapochukua tu hatua hivi..huh huh huh..
Msitari wa 6 na 7 tunaona jambo kubwa sana Mungu alilotenda walipotoka kwenye mazoea
*2 Wafalme 7: 6-7*
_6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi._
_7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao._
Mungu aliwasikizisha Jeshi la Washami wakasikia kishindo cha farasi na jeshi kubwa kumbe ni Wakoma wanne tu ambao walikuwa wamechoshwa na hali ilivyo wakaamua kutoka kwenye mazoea.
Na tunaona walivyochukua hatua wakaleta suluhisho la changamoto iliyokuwa imeikumba Samaria.
Mpendwa je ni jambo gani limekuchosha? Linakukera unatamani kuona mabadiliko?
Yamkini ni kwenye familia yako, au ndoa yako au kazini, biashara, shuleni au kwenye jamii.
Je unajua wewe ndio suluhisho la hiyo kero?
Je unajua jamii inapita kwenye changamoto kwasababu umeamua kukaa kwenye mazoea?
Leo Mungu anakuita utoke kwenye mazoea, ondoka kwenye comfort zone
STRETCH....
CHUKUA HATUA
Usingalie madhaifu uliyonayo,
Usiangalie ulishakosea mara ngapi,
Achana na historia yako mbaya,
Usiangalie watu watakavyokusema vibaya,
Chukua hatua, toka kwenye Comfort zone,
hayo mabadiliko hutayafanya mwenyewe, Mungu anatafuta tu mtu aliye tayari ili akutumie kuleta mabadiliko,
Unapochukua hatua ndio anakuvisha uwezo,
Anasikizisha adui zako kishindo hata kama huna vigezo watu wakiangalia CV yako wanatetemeka na wanakuta wamekupa hiyo nafasi,
Mungu anasikizisha kishindo cha kampuni yako hata kama ni changa wanakupa hiyo tenda,
Mpendwa chukua hatua,
Ondoka kwenye mazoea, Mungu atafanya mambo mengi makubwa ukimruhusu
STRETCH WOMEN SUMMIT TULIYOIANDAA ITAFANYIKA *TAREHE 21 NOVEMBA 2020*, Golden Jubilee Towers, PSSSF Building, 5th Floor
Uwe na Wiki ya Ushindi!
Mawasiliano
+255 754 934693