VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
_By Luphurise Mawere_
*11. Tambua Nyakati na Majira*
_Mwanzo 41: 28 -32_
_28 Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu._
_29 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri._
_30 Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi._
_31 Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana._
Pia soma _Mhubiri 3: 1-8_
Maisha yana Majira na Nyakati
Kuna wakati wa Kuzaliwa na wakati wa Kufa
Kuna wakati wa Kucheka na wakati wa Kulia
Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna
Pia kuna wakati wa SHIBE na wakati wa NJAA NZITO
Sijui uko nyakati gani mpendwa lakini Biblia inaniambia kwamba yako majira yanakuja kwahiyo usifikiri majira uliyoko utakaa hapo siku zote kwahiyo yakupasa kujipanga sawasawa
Kama uko kwenye shibe usijisahau maana yamkini Ibilisi anakuandalia mchakato wa kukuingiza kwenye njaa nzito
Lakini pia kama uko kwenye njaa nzito Jipe moyo utavuka hayo ni majira tuu
Je uko kwenye vipindi gani?
Umefilisika?
Biashara zimekufa?
Umepoteza kazi?
Kampuni yenu imepunguza wafanyakazi au imefungwa kabisa kwasababu ya Corona?
Ulikuwa na mali nyingi zimechukuliwa zote na Bank au wakopeshaji?
Yamkini umebakia makumbusho yaani kwamba unasimulia tu nilikuwaga na majumba, magari, nilikuwa nakaaga masaki, nilikuwa na fedha nyingi lakini sasa sina hata kitu,
JIPE MOYO Mpendwa hayo ni majira tu
Mungu bado anakupenda wala hajakukomesha na anakuwazia mawazo ya amani kabisa
Mara nyingine unaweza kupitia nyakati za Njaa nzito ili ufinyangwe kuwa yule Mungu aliyekukusudia sawasawa na _Isaya 64: 8_
Stahimili mpendwa
Utavuka hapo kwa ushindi mkubwa sana
_Warumi 8: 18 Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu._
Hiyo Njaa nzito unayopitia si kitu ulinganisha na vitu vitakavyozaliwa
Kama utaamua kukung'uta mavumbi na kuinuka ziko fursa, mawazo na mambo mengi mazuri yanazaliwa ambayo ni makubwa mno kuliko hizo changamoto
SONGA MBELE
WEWE NI SHUJAA!
Uwe na Wiki yenye Ushindi tele
Masomo yote yaliyopita yako kwenye link hii
+255 754 934693