VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
_By Luphurise Mawere_
*10. Tangaza Vita Vya Madeni*
_Nehemia 5: 1-5_
1 Ndipo kukatokea kilio kikuu cha watu, na wake zao, juu ya ndugu zao Wayahudi.
2 Maana, walikuwako watu waliosema, Sisi, na wana wetu na binti zetu, tu wengi; na tupate ngano, tule, tukaishi.
3 Tena walikuwako wengine waliosema, Tumeweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu, na nyumba zetu; tupate ngano, kwa sababu ya njaa.
4 Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu.
5 Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu.
Madeni ni kinachokosesha raha sana hapa duniani
Wayahudi walikuwa hawana raha tena kwasababu ya madeni, walikuwa wanalia maana wamakwama wamepoteza kila kitu walikuwa wameweka rehani na kukopa fedha matokeo yake wakawa utumwa
Mpendwa wangu madeni sio kitu cha kuchekea kabisa
Madeni yanaleta;
▪Magonjwa
▪Msongo wa Mawazo
▪Kufilisika
▪Kifungo
▪Kupoteza mahusiano
▪Kupoteza maisha
▪Utumwa -Slavery
▪Dhambi
▪Kudhalilika
Ndio maana inabidi kutangaza VITA ya madeni
*Kwanini watu wanaingia kwenye madeni*
▪Maisha ya kuiga na Mashindano
▪Tamaa
▪Kutaka kuonekana
▪Ujinga na Kukosa maarifa
▪Kuwa na matumizi mabaya
▪Marafiki wabaya
*Namna ya kutoka kwenye madeni;*
▪Ongeza kipato usiwe na kipato kimoja
▪Uza kitu ambacho ukihitaji
▪Bana matumizi
▪Anza kulipa madeni madogo halafu utamalizia makubwa
▪TANGAZA VITA YA MADENI USIINGIE TENA KWENYE DENI LINGINE
_USIKOPE DENI KULIPA DENI HUO NDIO UTUMWA WENYEWE_