Listen

Description

Zaburi 138: 7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa._

Soma pia _2 Mambo ya Nyakati 20: 1-30_

Tunaishi katika Ulimwengu uliojaa shida na taabu nyingi. Tuko kwenye Majira ambayo dunia imegubikwa na hofu na huzuni kubwa kwasababu ya shida ya janga la Corona, changamoto za upumuaji na tauni vinavyomaliza watu.
Watu wengi wamekosa tumaini kwasababu wapendwa wao wamepoteza maisha au wengine wako mahtuti kwasababu ya janga hili.
Ukifungua vyombo vya habari na ukiangalia mitandao ya kijamii imejaa habari mbaya za vifo. Watu wengi wanaona mwisho wa dunia umefika. Wanaogopa.
Nyakati kama hizi alipitia mfalme Yehoshefati kama tulivyosoma 2 Mambo ya Nyakati 20: 1-30. Maadui wakubwa watatu waliungana ili kuipiga Yuda aliyokuwa anaiongoza Yehoshefati mfalme, aliposikia habari hizi aliogopa sana kwasababu hakuwa na uwezo wa kupigana na maadui hao.
Dunia sasa tunaogopa maana janga hili tunalipitia hatuna uwezo wa kupambana nalo kwa hali yetu ya kibinadamu.
Kama familia yako imeguswa na janga hili utanielewa vizuri namna ambavyo watu wanakuangalia kwa huruma na hofu maana hawajui kama utavuka kwa namna ambavyo tumeona likimaliza familia hasa wale waliouguza wagonjwa. Ni kipindi kigumu mpendwa. Mungu peke yake ndio wakutuvusha hapo.
Ninajua kwa kiasi uharibifu unaoletwa na janga hili kwenye maisha ya watu, nilikaa hospitali na mgonjwa, nilienda ICU mara kadhaa niliona namna watu wamepoteza tumaini kwasababu ya maumivu makali. Inafika mahali wataalamu wa afya wanakuambia mpendwa tunafanya kila tunachoweza ila nawashauri mumuombe tu Mungu.
Najua nilikuwa exposed na kuumizwa sana na shida hii kwa kumpoteza mama sio tu kihivihivi najua kabisa ni kwa majira haya na namuomba Mungu anisaidie niweze kusimama mahali palipobomoka

*Vitu vitakavyotusaidia tuweze kuvuka katika shida au janga hili*
▪Usiogope
2 Timotheo 1: 7
Epuka kabisa hofu mpendwa wangu, hofu haitoki kwa Mungu, hofu ni ya shetani. Yeye hutupa hofu ili aweze kututawala vizuri na kutufanya tufuate njia zake ili atumalize vizuri.
Watu wengi niliowaona hospitali wamepoteza kabisa tumaini, wana hofu kubwa.
Tumepoteza watu wengi kwasababu ya hofu
Na hofu huwa inakuja pale ambapo tunatoa macho yetu kwa Mungu na kuweka macho kwenye tatizo.
Mpendwa toa macho yako kwenye matangazo ya vifo, hali unayoisikia na kuiona weka macho yako kwa Mungu aliye mkuu kuliko tauni, corona, kansa na shida yoyote ile.

▪Elekeza uso wako kwa Mungu
Mtafute Mungu kama Yehoshefati mfalme alivyofanya wakati anapitia wakati mgumu.
Kama ulikuwa hujui kuomba hiki ni kipindi cha kujifunza kuomba tena sio kuomba kirahisirahisi kuomboleza haswaa sawasawa na *Yeremia 9: 17-22*
Ni wakati wa macho kuchurizika machozi, kope kububijikwa maji.
Viongozi wa Taifa, Kanisa, Familia, wakubwa kwa wadogo huu ni wakati wa kuomboleza maana shida hii ni kubwa sisi hatuiwezi, Mauti imepanda madirishani kwetu!
Kama ulikuwa huendagi kanisani huu ni wakati wa kutafuta kanisa linalohubiri kweli ya Mungu ujiunge nao
Haya sio majira ya kusema watu watakuonaje wakijua wewe tajiri, Mkurugenzi, Mtu mwenye ushawishi unaomba na kumuangalia Mungu.
Huu ni wakati wa kufunga mpendwa, Yehoshefati aliitisha mfungo kwa Yuda yote.
Jifunze kufunga kama haikuwa tabia yako, anza kidogo kidogo.
Kufunga kunaonyesha utii kwa Mungu wako na ni njia ya kutoa mwili wako kuwa dhabihu takatifu mbele zake.

▪Mtumaini Mungu peke yake ndio mwenye suluhisho la shida unayopitia
Yehoshefati na watu wake walimtumaini Mungu peke yake kwenye vita iliyokuwa inawakabili na Mungu aliwapigania.
Wao hawakupigana Mungu ndio aliwapigania
Mpendwa hakuna Sayansi, Dawa, Uchawi, Taifa lenye nguvu juu ya janga hili. Tumeona hata Mataifa yenye Teknolojia kubwa za afya yakipoteza maelfu ya watu. Janga hili kubwa litamalizwa na Mungu mwenyewe.
Usiweke tumaini lako kwenye barakoa, kujifukiza, sanitizer, Dawa au kituo fulani cha afya ndio unawez