Listen

Description

UKIZIMIA SIKU YA TAABU NGUVU ZAKO NI KIDOGO
_By Luphurise Mawere_

_Mithali 24: 10 Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache._

Tunaishi katika dunia ambayo imejaa taabu nyingi. Vyombo vya habari kila mara vinatoa taarifa za taabu katika mataifa mbalimbali, utaona Taifa hili likipita katika taabu moja hadi nyingine.
Lakini watu pia wanapitia taabu mbalimbali. Yamkini unapitia ujumbe huu uko kwenye taabu nzito; labda umeondokewa na mpendwa wako, umetelekezwa na mwenzi wako, umesalitiwa na mwenzi au mchumba wako uliyempenda na kumwamini sana, au mtoto wako amefanyiwa vitendo viovu vya udhalilishaji kijinsia, au umebakwa, au nyumba yako imeungua yote, au umefilisika, umefukuzwa kazi, umelala kitandani kwa ugonjwa unaokutesa wamekuambia hauna tiba, au Madaktari wamekuambia huwezi kupata mtoto. Mpendwa kwanza pole sana kwa hayo unayopitia
Ila leo neno la Mungu linakujia kukuambia kwamba pamoja na yote hayo unayopitia usizimie, usikate tamaa, jitie nguvu katika Bwana maana yeye yuko upande wako.
Maneno ya Mungu katika _Isaya 41: 10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu._
Mpendwa wangu hiyo taabu unayopitia sio mwisho wa hatma yako,
Usizimie
Usifadhaike
,Bado liko tumaini,
Jitie nguvu kwa Bwana, yeye yuko upande wako, anakupenda, atakutia nguvu na kukusaidia ili uvuke salama,
Usipigane mwenyewe, hiyo vita siyo yako acha Mungu wetu mzuri akupiganie
Tiwa nguvu mpendwa wangu
Kama ukikuwa umejikunyata, au umejifungia ndani, au hutaki kuongea na mtu hebu INUKA toka nje kwa UJASIRI sasa,
_Zaburi 34: 17 Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya na taabu zao zote._
Hebu amua kutoa macho yako kwenye hiyo taabu, weka macho yako kwa Mungu ambaye yuko juu ya hiyo taabu, yeye atakuponya na taabu zako zote
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana, ataiondoa hiyo taabu hata kama dunia nzima imesema haiwezekani
Usizimie siku ya taabu, jitie nguvu katika Bwana . Mawasiliano +255 754 934693