VITU VYA KUFANYA ILI UWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
_By Luphurise Mawere_
*9. Usitapanye Mali na Pesa Mungu alizokupa*
_Luka 16: 1-12_
Mungu anatutaka tuwe mawakili wema wa mali na pesa alizotupa,
*Wakili* ni mtu anayesimamia mali za mtu mwingine,
Sisi ni mawakili wa vitu Mungu alivyoweka kwenye maisha yetu,
_Mwanzo 2: 15 BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza._
Mungu alimweka Adamu pale bustani ya Edeni kuitunza, haikuwa mali yake hivyohivyo kazi, biashara, nafasi na pesa tulizonazo sio zetu Mungu ametupa ili tu tuzisimamie sisi ni Mameneja yaani Mawakili tu,
*Sifa za Wakili Mwema*
▪Anatambua Mungu ndie mwenye pesa, mali na kila kitu alichonacho yeye ni msimamizi tu
▪Anaweka akiba, hatumii kila kitu anachokipata
Watu wengi hatuna tabia ya kuweka akiba tunatapanya kila kitu,
_Mithali 6:6-8_ inatuambia tujifunze kwa chungu yeye ni mdogo mno na hana akida lakini anajua kuweka akiba
▪Anabana matumizi ya simu, vyakula, fashion, sherehe, TV na mitoko mbalimbali
▪Sio mbinafsi maana anajua vitu vyote ni vya Mungu
▪Anaepukana na mashindano na mikumbo itakayompelekea kwenye kutapanya
▪Hanunui vitu ambavyo havihitaji, haongozwi na tamaa
▪Ni mwaminifu kwenye kidogo Mungu alichompa mf.pesa, mali, kazi, biashara
Mungu akusaidie uwe wakili mwema, Usitapanye Mali alizokupa
Halleluya!
Mawasiliano
+255 754 934693