Kuna wakati inakulazimu uachane na mshirika wako (Business partner) ambae mlikua na Malengo ya kufika mbali sana kutokana na malengo mliyojiwekea.
Kuna wakati inakubidi uachane na bosi wako ambaye ndie aliekusaidia kukufundisha kazi hapo mwanzo na mpaka ukawa imara.
Kuna wakati ni lazima tu uachane na mtu uliekua unampenda sana, na ulidhani ungekuwa nae kwa kipindi chote cha maisha yako duniani.
Vile vile kuna wakati katika maisha utatakiwa uachane na watu, ofisi, au chama cha siasa hata kama ulikua unawategemea.
Sasa ukifika wakati huu kuna mambo ya KUZINGATIA.
1. Sio lazima UANZISHE UGOMVI na unaoachana nao.
Unaweza kuachana nao kwa HESHIMA na UTULIVU bila migogoro ya aina yoyote.
Kumbuka kuachana sio VITA, kwani mnaweza kuachana na maisha yakaendelea kama kawaida.
Sio lazima uwageuze UADUI wale unaowaacha au wanaokuacha.
Maisha yana Wakati au Majira na kila mtu anatakiwa kuwa sehemu fulani kutokana na wakati fulani.
2. Pokea MAUMIVU na YAKUBALI, kwani haitasaidia kutokukubali uhalisia.
Kama mtu ameamua kuondoka hakuna namna.
Haitasaidia kukataa uhalisia, badala yake jipange kwa yanayofuata.
3. USIJILAZIMISHE kuonesha UBAYA kwa unaeachana nae.
Kumbuka mafanikio ya unapokwenda HAYAJABEBWA na watu kujua ubaya wa UNAEACHANA nae, bali YANABEBWA katika dhamira safi ya UNACHOKWENDA KUFANYA.
Hakuna umuhimu wa kumpaka matope unaeachana nae.
KUACHA au KUACHWA inaumiza sana lakini hakuna namna ni lazima maisha yaendelee.