Mkoa wa Nagaland unaopatika mashariki mwa India imepiga marufuku uuzaji wa nyama ya mbwa iliyokua inafanyika kwa muda mrefu.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na jarida la The Indian Express, ni kwamba katibu wa jimbo la Temjen Toy nchini India amesema kwamba Serikali yake imechukua uamuzi wa kupiga marufuku biashara ya kuuza nyama ya mbwa kwa hali yoyote.
Siku zote nyama ya mbwa imekua ikiliwa kitamaduni katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa India.
Baadhi ya mashirika ya kiraia katika maeneo hayo yamekemea uamuzi huo wakati ambapo shirika la kimataifa la haki za wanyama limepongeza uamuzi huo uliochukuliwa na serikali.
Zaidi ya mbwa 30,000 kila mwaka huuzwa katika masoko ya majimbo hayo ambayo yana utamaduni wa kula mbwa kaskazini mashariki.