Listen

Description

Utakubaliana na mimi kwamba kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiari kwamba sasa mtu anaamua ngoja sasa nibanwe na mkojo,hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda,au vinywaji tunavyotumia.Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature's call.

Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini,akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, Mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kupunguza maji hayo kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza wito huu wa asili.Mambo haya tunayafanya sana utasikia mkojo umebana kweli ila ngoja nimalizie hii kazi alafu nitaenda kujisaidia hivi ndiyo watu wengi wanafanya.

Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo mkojo unapofika karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa.Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili RECEPTORS vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, Baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.

Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani,automatic kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwakuwa Ubongo nao hutuma taarifa kwenye kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo utashindwa kufanya kazi ya kutoa taarifa au uwezo wa ubongo kuwa mdogo,Na matokeo yake itakuwa huwezi tena kuvumilia hata kwa muda ulio mdogo na utajikuta unajikuta umeshalowanisha nguo.

Madhara mengine ni kwamba mtu akibana sana mkojo kwa muda mrefu na mkojo ukashindwa kutoka kwa wakati basi ni wazi kupata magonjwa kama U.T.I na pia utasababisha ugonjwa wa kibofu(bladder infection), Magonjwa ya figo na machafuko wa damu, bacteremia.

Mpenzi msomaji ni vyema tukawa wasikivu pale mtu anapobanwa na mkojo,hii ni kwaajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwaajili ya afya yako kwa ujumla, kama unalo tatizo usisite kuonana na wataalamu wa afya.