Listen

Description

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amethibitika kupata maambukizi ya virusi vya Corona, baada ya kuwa na tabia ya kupuuzia ugonjwa huo kwa kuuita mafua tu yasiyokuwa na athari kubwa.

Taarifa ya maambukizi ilianza tangu siku ya Jumatatu baada ya kupimwa na kukutwa na kiwango cha juu cha joto.

Aidha Jair Bolsonaro pia alikua amewataka magavana kulegeza masharti yaliyowekwa kama njia moja ya kukabiliana na Ugonjwa wa virusi vya Corona akisema kuwa hatua hizo zimeathiri uchumu, huku yeye mwenyewe siku hiyo ya Jumatatu akisahau kuvaa Barakoa.

Rais huyo wa Brazil alishawahi kusema kuwa hata kama akipata Corona, hatakuwa na wasiwasi wowote sababu zaidi itakua ni kama mafua tu au homa.

Alipokua anatoa hilo tangazo, idadi ya waliothibitika kupoteza uhai kutokana na maambukizi ya Covid-19 ilikua bado ni chini ya 3,000 huku maambukizi yakiwa ni 40,000, lakini idadi imekua ikiongezeka tangu wakati huo.

Lakini licha ya idadi kuzidi kuongezeka Rais Bolsonaro amekua akisema kuwa athari za kufungwa kwa maeneo ni kubwa sana kuliko za virusi vyenyewe, na kuvishutumu vyombo vya habari kwa kusababisha hofu kwa raia wake.

Mpaka sasa idadi ya waliofariki nchini Brazil imeshafikia 66,868 huku waliopona wakiwa ni milioni 1.7 na waliothibitika kuwa na maambukizi ni milioni 1.67, lakini Taifa la Marekani likiwa linaongoza kwa kuwa na maambukizi Milioni 3.5, waliopona ni 918,000 na waliofariki ni 133,000.