Mara nyingi kama vijana tuna kasumba potovu eti wale wanaostahiki kuwekeza pesa ama rasilimali ni wazee.Huu ni uongo mtupu!Vijana wanapaswa kuanza kuwekeza mapema ili wakati wanastaafu,wana akiba ya kutosha.Ni changamoto sisi sote kujifunza kuwekeza ili uzeeni uishi maisha marefu.Yakini,chelewa chelewa utapata mwana si wako.