WOKOVU ni hatua ya kwanza. Mkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Kuwa mwaminifu kwa MUNGU. Acha dhambi sasa. Ishi maisha ya utakatifu.
Msikie MUNGU na kuitii sauti yake. Amekuita kumtumikia, usikimbie itikia wito. Kuwa mtu wa toba wakati wote. Tenda wema bila kuchoka. Kila mara tafuta fursa ya kutenda wema kwa mwingine. Kuwa na HESHIMA na KUWATHAMINI WENGINE kwa kutambua ya kuwa kila mmoja ana thamani mbele za Mungu kulingana na neema tofauti ambazo kila mmoja amebarikiwa na zote zina thamani
1 Wakorintho 6: 9-10
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
UKO TAYARI KWA AJILI YA SIKU HII? HEBU FUNGA MACHO NA YATATHMINI MAISHA YAKO SASA. UTAVUKA? UCHAGUZI UNAFANYA SASA HIVI, SIO KESHO. Maana MWISHO wako unaweza kuwa NUSU SAA ijayo. UMEJIANDAAJE?
Kama uko tayari kuacha njia zako mbaya na kutengeneza na MUNGU tutumie ujumbe kwenye whatsapp +255754440139.
FANYA MAAMUZI SAHIHI.
🎶 🎶 🎶
HIMA NDUGU TUINGIE, LANGO HALIJAFUNGWA
LIKIFUNGWA MARA MOJA, HALITAFUNGULIWA
MAANDIKO ZAIDI
Ufunuo wa Yohana 20: 11-15
Mhubiri : 12: 14
2Petro 3:3-18
Mathayo 25: 31-41
“2021, MFUATE YESU, SIO DUNIA”