JINSI GANI KIJANA AISAFISHE NJIA ZAKE
01.KWA KUTII
02.KULIFATA NENO
Mhubiri 12:1 '' Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. ''
Ni muhimu sana kwa kijana kumcha BWANA tangu mapema kabisa katika umri wake maana Kijana Asiyezoea Kujizuia Kimwili Kabla Ya Ndoa, Hataweza Kujizuia Katika Ndoa. Wasaliti Wengi Wa Ndoa Zao Ni Wale Ambao Hata Kabla Ya Ndoa Walishindwa Kujizuia Miili Yao Na Kuwapelekea Kufanya Uasherati. 2 Timotheo 2:22 '' Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi. ''
Baada ya kijana kumkumbuka MUNGU kwa kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha ya Wokovu, Biblia inashauri kijana kuanza kuliishi neno la MUNGU, Kulifanya taa ya miguu Neno ili limuongoze kijana katika matendo mema na kumtii MUNGU siku zote. Zaburi 119:105 '' Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. '' . Neno la MUNGU likiwa muongozo kwa maisha ya kijana kutakua na ushindi mkubwa sana kwa kijana huyo. Njia ya maisha ya kijana lazima iwe safi ndipo atampendeza MUNGU, Njia itakuwa salama kwa kijana kulitii tu neno la MUNGU(Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.-Zaburi 119-9)
Tena Wana Amani Nyingi Wasiokwazwa Na Maonyo Ya Neno La MUNGU (Zaburi 119:165, Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza. ).