Nimewaandikia ninyi vijana,Kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu,nanyi mmemshinda yule mwovu.Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia.Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.Maana kila kilichomo duniani, yaani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima havitokani na Baba. bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu atadumu hata milele. {1yohana 2;14-17}
Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako, uchangamke wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na upeo wa macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu kadiri ya hayo yote. Ondoa mahangaiko moyoni mwako, jikinge, usipate maumivu mwilini kwa sababu ujana na mwisho wa maisha ni bure kabisa.