Listen

Description

Ndoto ni muhimu sana katika ulimwengu wa roho. Tunapokuwa tumelala, miili yetu ndo inalala lakini roho zetu hazilali. Hivyo kunakuwa na mambo mengi ambayo yanakuwa yanatendeka katika ulimwengu wa roho.

Somo la ndoto ni somo pana sana na ni vigumu kuliandika nikagusia kila kipengele. Hivyo lengo la post hii ni kukupa mtaji ili uweze kuelewa maana ya baadhi ndoto chache ambazo umekuwa ukiota. Hii itakusaidia unapokuwa unaomba kwani unahitaji kuelewa unachoombea. 

Kama nilivyosema mwanzo kuna ndoto za kutoka kwa Mungu (Matendo 2:17), ndoto za kutoka kwa shetani (Ayubu 7:14—15), na pia kuna ndoto ambazo ni matokeo ya shughuli nyingi.  “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi” (Mhubiri 5:3).