Kila kitu kwenye maisha ya mwanadamu kimebebwa na WAKATI. KUSUDI la wewe kuwa duniani limebebwa na WAKATI. Ni TIMELINE ya maisha yako mpaka siku ya mwisho. Timeline maana yake ni
MUDA => TUKIO.
1965 => KUZALIWA
2007 => KUFA
KUZALIWA na KUFA, hayo ni MATUKIO mawili makubwa yaliyopo kwenye timeline ya kila mwenye PUMZI. KATIKATI hapo kuna matukio mengine, yaliyoambatana na muda kulingana na KUSUDI na mapenzi ya MUNGU kwenye maisha yako.
Kama vile ambavyo matukio mbalimbali yametokea na kubadilika kwenye maisha yako, yani ulizaliwa, ukakua na sasa uko hivyo jinsi ulivyo; hiyo ni timeline yako inazidi kusogea, sasa hatujui kama timeline yako na ya MUNGU juu yako zinafanana au uliamua kutengeneza ya kwako, sasa hilo ni somo la siku nyingine. BASI uwe na UHAKIKA kabisa kuna MWISHO wa WEWE kuwa hapa duniani. Baada ya MWISHO au KIFO hakuna kingine kinachofuata bali ni HUKUMU (Waebrania 9:27)
HUKUMU ni TAMKO ambalo kila mmoja atapokea kama IJARA ya mambo aliyotenda akiwa duniani, kwa kadiri alivyotenda, kwamba ni MEMA au MABAYA(2Wakorintho5:10).
HIYO siku hakutakuwa na nafasi ya kujitetea. Hakuna kusema nilikuwa sijui, kwasababu kila mwenye pumzi lazima aisikie INJILI, ni yeye mwenyewe kuamua kuamini au kutoamini. Hiyo siku hakutakuwa na KUKATA RUFAA. Hukumu ikitoka imetoka. Wala pesa hazitafanya kazi kwako. Hakutakuwa na rushwa. Wala hakutakuwa na MATABAKA, kwamba huyu alikuwa raisi, waziri, celebrity, bongo movie maarufu, huyu alikuwa na followers milioni 8, huyu alikuwa miss Tanzania, huyu alikuwa na tuzo lukuki, huyu alikuwa mfanya biashara maarufu. Hakutakuwa na “wakili msomi” wa kukutetea, kwasababu hata yeye atasimama kwenye kiti cha hukumu ahukumiwe, kama alidhurumu watu basi hiyo siku itajulikana. Hapo ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno.
“Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno” (Mathayo 13:49-50)
MUNGU ANASISITIZA KUGEUKA kwa wanadamu na kusisitiza juu ya NYAKATI za mwisho. Na kila mmoja AKAIONE neema ya MUNGU na UPENDO WAKE ili asiangamie siku ya mwisho.
ENDELEA KWENYE POST INAYOFUATA