Hivi unajua kuna Marafiki ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kubwa maishani pia kuna aina ya Marafiki ukiwa nao ni mwanzo wa kukaribisha majanga.
Unajua kwamba...
Wewe ni wastani wa Marafiki sita ambao unashinda nao muda mwingi.
Hata kama hupendi au hauna marafiki, lakini bado unahitaji watu si ndiyo?
Na watu hawa wakiwa na sifa fulani fulani ni Muhimu kuwatunza maana tupo zama tumezungukwa na Marafiki au watu ambao ni wanafiki sana...
...kuna aina tano za Marafiki ambao ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kutoka wa Mungu maana ni Adimu zaidi ya Dhahabu kwenye machimbo ya Chunya pale Mbeya.
Ha!Ha!Ha! Unacheka au sio.
Hivi...
Ukiwa na rafiki ambaye anakuambia ukweli ambao unakujenga unajisikiaje? Jibu unalo.
Je, Ukiwa na rafiki ambaye anakupongeza unapofanya vizuri unajisikiaje? Jibu unalo.
Je, ukiwa na rafiki ambaye ni balozi wa kutangaza mazuri na kukunganisha kwenye Fursa na connection za faida?.
Majibu ya maswali umeshapata na unagundua unaweza kuwa unao au hauna. Sio tatizo kubwa.
Unashanga si ndiyo eeh...!
Ni hivi...
Haijalishi uko wapi na unafanya nini kama ni sehemu ambayo watu wapo basi unahitaji ukipata kati ya aina tano hizi za Marafiki basi usiwapoteze kabisa maana ni zaidi ya Tanzanite...
...pale machimbo ya Mererelani Arusha.
Unataka kuwajua aina hizi za marafiki.
Hata usiogope...
Ndiyo maana,
Nimekuandalia episode ya moto sana katika “Maisha Ni Kuthubutu Podcast” ujifunze zaidi kwa urahisi na kuelewa kwa kina.
Baada ya Kusikiliza pengine utajutia kwanini sikuiweka episode hii mwaka mmoja au miaka iliyopita! Muda sahihi ni sasa ndio sababu ya kusoma hapa.
Una sekunde 4 tu za kubofya link hapa chini Kusikiliza episode hii ili ujue aina 5 za Marafiki ambao ukiwa nao usiwapotezee.