Listen

Description

Mahusiano hayawahi kuwa mabaya hata siku moja, shida ni watu ambao wanaingia kwenye mahusiano.

Hivi Mahusiano ni nini?

Lakini...

Hakuna maana rasmi ya mahusiano kwa sababu kila mtu ana tafsiri yake, lakini tafsiri yako ni sahihi au ya kufuata mkumbo.

Leo hii imekuwa ni kawaida...

Kusema wanaume wote ni mbwa kwa sababu ya mwanaume mmoja kukusaliti kwenye mahusiano.

Kusema wanawake wote ni malaya kwa sababu ya mwanamke mmoja kukufanyika tafrani kwenye mahusiano kiasi unawachukia wanawake wote.

Umewahi kusikia Tanga wanasema “Mahusiano ni matamu kama asali mkiwa mnapendana”...

...vijana wanasema “Tanga ndiyo mapenzi yaliyokazaliwa” wana maneno sana, hahaha!

Ngoja nikuambie ukweli tu...

Mahusiano kuna vitu hupaswi Kulazimisha badala yake ni kujua wajibu na vinakuja “Automatic”.

Swali la kujiuliza...

Je, mahusiano yako mnapendana au mnalazimishana?

Huwezi kulazimisha upendo.

Huwezi kulazimisha kupewa muda “Quality time”.

Huwezi kulazimisha mahusiano.

Huwezi kulazimisha mtu kujitoa kwa ajiki yako.

Ndiyo sababu ya kufanya podcast ya dakika 16 za kuponya mahusiano sahihi ambayo yameyumba

Au

Mahusiano ambayo siyo sahihi nini ufanye ili usiendelee kupoteza muda wako.

Sikiliza hii episode ya 11 ya “Mambo matano (05) ambayo hupaswi kulazimisha kwenye mahusiano”.

Unataka Kusikiliza na Upo tayari? Ni rahisi sana cha kufanya ni kubofya link hapa chini na usikilize...