Listen

Description

Unaweza kutimiza malengo yako, kama utajua mbinu sahihi ambazo ni chachu ya kutimiza malengo yako.

Lakini...

Kuna sababu ambazo zinafanya watu wengi washindwe kutimiza malengo yako, inawezekana hata wewe mwaka 2022 ulishindwa kutimiza malengo yako kwa sababu fulani fulani si ndiyo?

Kutimiza malengo siyo ajali bali ni mchakato mtalaamu.

Kati ya sababu hizi inaweza kuwa chachu ya kushindwa kutimiza malengo yako;

1. Kutojua umuhimu wa kuwa na malengo,

Unaishi kwa mazoea kutojua umuhimu wa malengo, kwa sababu Hakuna shule au chuo inafundisha umuhimu wa kuishi kwa malengo katika maisha yako, na kuishia kuwa na ndoto na matamanio tu.

2. Kutojua umuhimu wa kupanga malengo yako,

Kwa sababu wengi hudhani wana malengo SMART kumbe wana ndoto na matamanio tu, katika Podcast ya maisha ni Kuthubutu nimeleza namna ya kupanga malengo SMART kwa kina, chukua muda sikiliza.

Jiulize maswali yafuatayo;

Je, malengo yako umeandika?

Je, umeweka mipango thabiti?

Je, umeweka deadline kujua lini utatatimiza malengo yako?

Je, umevunja malengo makubwa kwenda malengo madogo madogo?

Je, unajua hatua gani uchukue ili utimize malengo yako?

Ni baadhi ya maswali ambayo ni Muhimu kujiuliza wakati unapanga malengo yako?

3. Hofu ya kufeli,

Kuna Hofu ya kuanza na Kuthubutu kupambana kutimiza malengo yako, kuna Hofu inafanya ushindwe kupiga hatua, Je unajua hofu inayokusumbua?

Kwahiyo...

Ni baadhi ya sababu ambazo zinafanya ushindwe kutimiza malengo yako, baada ya kujua sababu hizi umekuwa chachu ya kutimiza malengo kwa asilimia 94% na zaidi

Kwa sababu nataka utimize malengo yako kutoka sasa si Upo tayari si ndiyo eeh! Basi ni simpoooo...

Bofya link hapa chini Kusikiliza episode ya 18 hapa chini una dakika 18 za kutimiza malengo yako kuanzia sasa na kuendelea...