Ni nadra kwa muhitimu kupata nafasi ya kazi haraka pindi tu anapojinyakulia stakabadhi zake za chuo kikuu au hata cha kati hivyo basi wengi wa waliohitimu huamua kuingia katika biashara ili kuendelea kukimu mahitaji yao na hata kulipa mikopo waliochukua ili kulipa karo zao.