Ni Mtaa wa Ziwa mkoani Mwanza ambao umeharibiwa huku nyumba za wakazi wake zikizama kwenye maji baada ya kina cha maji cha Ziwa Victoria.
Kuongeza kwa kina cha maji cha ziwa hilo ni matokeo ya uchafuzi wa mazingira, mafuriko na mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2020. Wadau wa mazingira washauri watu kuondoka katika mtaa huo huku wakihimiza watu kuacha kujenga au kufanya shughuli za kilimo na uzalishaji ndani ya mita 60 ya vyanzo vya maji ili kuepuka madhara.
Kufahamu zaidi, sikiliza makala haya yanayoleta kwenu na Herimina Mkude.