Mwaka 2021 unavyoanza alikuwa ana matumaini lukuki kuwa ng’ombe wake aliokuwa nao wangechangia kwa kiwango kikubwa kumuongezea kipato na kumtoa katika umaskini.
Miezi 11 baadaye ndoto ya Ndirana Ndirana Jijungu, mkazi wa Kijiji cha Mwamihanza wilayani Maswa mkoani Simiyu ilizimwa ghafla kwa kupoteza ng’ombe wanne kati ya sita baada ya kukosa malisho kutokana na ukame. Hata hivyo, ukame wa mwishoni wa mwaka 2021 umemfanya apoteze sehemu kubwa ya mali na kumrudisha kwenye umaskini.
Tofauti na miaka mingine, mvua hizo zilichelewa kiasi cha kuathiri upatikanaji wa malisho na maji maeneo mengi wilayani Maswa, kama anavyosimulia Herimina Mkude.