Listen

Description

Mike, dereva taxi jijini Dar anambeba mteja wa kike, Natasha kumpeleka kwenye miadi yake usiku wa saa sita. Lakini anajikuta akiwa kwenye sehemu isiyo sahihi katika muda usio sahihi. Yeye na Natasha, wanakabiliwa na hatari kubwa kuwahi kutokea maishani mwao. Hawafui dafu mbele ya askari wa cartel kubwa Afrika Mashariki, Paka Weusi. Kwa pamoja wanajikuta kwenye Handaki la Kifo, jela maalum kwa waasi wa kundi hilo. Akiomboleza kifo cha kinyama cha mpenzi wake Ray, Natasha anabakiwa na kazi mbili kubwa – kulipiza kisasi cha mpenzi wake dhidi ya adui namba moja, Red Poison na kujiokoa kutoka kwenye sehemu hatari zaidi iliyo chini ya ardhi.