Makala haya ya Nyuwi si utsai ni makala kwa lugha ya kigiriama
kutoka jamii ya mijikenda yanayozungumzia kuhusu
kukomesha visa vya mauaji ya wazee kwa kisingizio cha uchawai.
Kwa zaidi ya miaka kama miaka mitatu iliyopita wazee wengi
katika kaunti ya Kilifi wamekua wakiuliwa kwa kusingiziwa kuwa ni wachawi hali
ambayo imeleta wasiwasi mkubwa kwa jamii ya kaunti hio.
Kila mwaka wazee 150 huuliwa hii nikulingana na shirika la utunzi
wa mila na damaduni za mijikenda MADCA .
Ndio sababu iliyonifanya kuzama na kuja na makala haya
ambapo niliongea na spika wabunge la kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire ambaye
anasema kuwacha mila na kukumbatia mila za kigeni ndio chanzo cha watu kuwaona
wazee kama tishio kwa maisha yao.
Pia ukosefu wa ajira nao umetajwa kuchangia kwa vijana
kutamani utajiri wa haraka bila jasho hali ambayo huwafanya kuwaua wazee wao
ili warithi mali.
Mzee Stanlus Kiraga wa MADCA anasema kuwa zamani ucgawi
ulikua ukitumika kulinda mamboma ya jamii ya mijikenda lakini siku hizi watu
wamekosa kuuelewa na wameanza kuwaroga wenzao.
Chidongo naye anasema vijana wakiota ndoto mbaya tu basi
huanza kuwashuku wazee wao hali inayochochea mauaji hayo.
Mwambire anasema watu wakija pamoja na kuelewa mila na
desturi za mijikenda hali hii itakomeshwa.