Rhapsodi ya Uhakika, Dec 5, 2020
Mpendwa Baba, ahsante kwa kuniita katika maisha ya athari na kwa kunipa rasilimali kuu kuliko zote—ambayo ni Roho Mtakatifu—ili kunisaidia kutembea katika mapenzi Yako na makusudi Yako kwa ajili ya maisha yangu. Uliniumba katika Kristo Yesu kwa ajili ya kazi njema ambazo uliziandaa tangu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu kwamba nienende katika hizo. Na sasa, kwa Roho Wako, maisha yangu yote yako katika kuliendea kusudi Lako na kutawazwa kwa Ufalme Wako katika mioyo ya wanadamu, katika Jina la Yesu. Amina.