Rhapsodi ya Uhakika - Oct 31, 2020
Pro 4:5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. Pro 4:6 Usimwache, naye atakuhifadhi; Umpende, naye atakulinda. Pro 4:7 Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu. Pro 4:8 Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia. Pro 4:9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji ya uzuri.