Rhapsodi ya Uhakika - Nov 9, 2020.
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu (1 Yohana 5:4).
Mimi ni shupavu katika imani na katika neema
ambayo iko ndani ya Kristo Yesu. Ninatamka ushindi,
mafanikio, afya, nguvu, na uhodari daima, kwa
maana mkuu ni Yule aliye ndani yangu, kuliko yule
aliye katika dunia. Neno la Mungu limeshika hatamu
yote na linadhihirika ndani yangu, na kupitia roho
yangu, nafsi, na mwili. Haleluya!