Mungu amejitukuza Mwenyewe ndani yangu; sasa,
ninaubeba utukufu huo kila mahali. Hakuna aibu
maishani mwangu; ninatembea katika utukufu, na
maisha yangu yamejawa utukufu—heshima, nakshi,
ukuu, uzuri, upendeleo! Ninatembea kiuendelevu
katika afya ya kiungu, ustawi, na kuiathiri dunia
yangu kwa utukufu Wake. Asifiwe Mungu!