Rhapsodi ya Uhakika: Oct 22, 2020
Yesu ni Mungu katika mwili wa binadamu, lakini watu hawakujua. Yeye ni Adonai, Yaani Bwana, Mungu! Ndiye aliyemwambia Musa, “Baba zako, Ibrahimu, Isaka na Yakobo walinijua kama, Mungu Mwenyezi (mweza wa yote), lakini mimi ni Yehova” (Kutoka 6:3). Yehova ni Yahweh.
Na kama haujawahi kuzaliwa mara ya pili, kama bado haujamfanya Yesu kuwa Bwana wa maisha yako, iseme sala hii na uimaanishe kwa moyo wako wote: “Ee Bwana Mungu, ninaamini kwa moyo wangu wote katika Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini alikufa kwa ajili yangu na ya kuwa Mungu alimfufua kutoka katika wafu. Ninakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, ninao uzima wa milele; nimezaliwa tena. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa mimi ni mtoto wa Mungu. Haleluya!”