Rhapsodi ya Uhakika - Oct 26, 2020
Baadhi ya watu wameutoa muda na mali zao katika kuhakikisha kuwa Injili inafika katika kila taifa la duniani. Wanafanya mambo makubwa katika kuiendeleza ajenda ya Mungu, wakiufidia upungufu na kutoweza kwa wengine. Wanatoa fedha nyingi sana katika kuisukuma Injili; na kadri watoavyo, ndivyo Bwana aelekezavyo zaidi rasilimali katika njia yao ili wakafanikishe mambo makubwa zaidi kwa ajili Yake. Atakusambazia yote utayoweza hitaji ili kulitimiliza kusudi Lake la kuvuna nafsi.