Rhapsodi ya Uhakika, Nov 23, 2020.
Jitahidi katika ubora wako usiiharibu siku ya wengine. Najua, kuna upande wa pili kwa jambo hili; unaweza kuwa ndiwe upaswaye kumuona mtu, lakini umeweka muda uo huo kuwaona watu wengine watano katika mji! Kwa hakika utakwenda angalau kumsubirisha mtu mmoja au zaidi kati yao, na hiyo si sawa. Hata ukiwa kama mkubwa (bosi) katika ofisi, kuwa makini na ratiba za walio chini yao. Watu waliofanikiwa wanajali [na kuzingatia] muda.