Listen

Description

Rhapsodi ya Uhakika - Oct 29, 2020.

Mithali 18:21 inasema, “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.” Utavuna mavuno ya mambo mema kupitia maneno yako. Maneno ni vitu; maneno ni nguvu ya uumbaji. Maisha yako leo ni matokeo ya maneno yako. Mithali 15:4 inasema, “Ulimi safi ni mti wa uzima….” Kama maneno yako ni mazuri, maisha yako yatakuwa makamilifu, bora, na ya kuhamasisha.