Listen

Description

Mchungaji Mmasa na Mwalimu Mike wanatoa maelezo ya Biblia katika waraka wa Paulo kwa Wagalatia. Tutafundisha waraka mzima sehemu kwa sehemu mwanzo hadi mwisho. Podi hii ya kwanza ni juu ya Wagalatia 1:1–9. Tunajifunza kusudi la Paulo kuandika waraka na hatari ya kuamini Injili isiyo kweli. Wagalatia walifundishwa Yesu hakuwatosha, bali lazima kuweka na tohara. Lakini Paulo alisema hayo ni uzushi na wakiamini mafundisho hayo watakuwa wamemwacha Yesu maana wanaweka imani katika Yesu pamoja na vitu vingine.

Karibu!

Wagalatia 1:1–9 (Soma Biblia hapa)

1 Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), 2 na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia; 3 Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo; 4 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu. 5 Utukufu una yeye milele na milele, Amina.

6 Nashangaa kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia Injili ya namna nyingine. 7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza Injili ya Kristo. 8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe. 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.



This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mwalimumike.substack.com