Habari wanamafanikio?
Karibuni kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo mwanamafanikio mwenzetu Johnbosco Boniphace anatushirikisha safari yake ya biashara.
Kwenye kipindi hiki utajifunza yafuatayo;
* Jinsi alivyoweza kukusanya mtaji kupitia fedha ya kujikimu chuoni
* Jinsi alivyoweza kutumia changamoto kuona fursa ya kuanzisha biashara.
* Jinsi alivyokuwa king'ang'anizi mpaka kupata eneo zuri la kufanyia biashara.
* Nidhamu yake ya hali ya juu katika kuendesha biashara yake.
* Upinzani kutoka kwa wengine kutokana na mafanikio anayoanza kupata.
* Kuzushiwa imani za kishirikina kutokana na hatua za tofauti anazopiga.
* Msukumo wa jamii kuhusu kupata ajira na jinsi ya alivyoweza kuvuka hilo.
* Malengo makubwa aliyonayo kwenye biashara.
* Ratiba yake ya siku katika kuendesha biashara yake kwa ufanisi mkubwa.
* Ushauri aliopata kutoka kwa wengine.
Karibu usikilize kipindi hiki, kina mengi ya kujifunza ambayo yatakusaidia kupiga hatua zaidi kimafanikio.
Kocha.