Listen

Description

Habari Mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kuna mambo makubwa mawili.

Jambo la kwanza ni uchambuzi wa kitabu cha BILLIONAIRE IN TRAINING. Hiki ni kitabu muhimu sana kwenye safari yetu ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha. Na ndiyo kitabu kitakachokuwa mwongozo mkuu kwetu.

Kwenye uchambuzi huo tutajifunza kuhusu utajiri na ukwasi na njia tatu za kupata utajiri na ukwasi. Na pia tutajifunza ngazi tano za ujasiriamali, kuanzia sifuri ambayo ni kuajiriwa, kisha kujiajiri, umeneja, umiliki, uwekezaji na hatimaye ujasiriamali.

Huu ni uchambuzi muhimu sana ambao pia utaendelea kwa kina kwenye kipindi kijacho cha ONGEA NA KOCHA. Hivyo usikubali kukosa kwa namna yoyote ile, maana huo ndiyo mkeka wetu wa kuelekea kwenye ubilionea.

Jambo la pili ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Helanane Ilomo ambaye anatushirikisha sehemu ya safari yake ya mafanikio.

Kwenye mahojiano hayo anatueleza jinsi alivyoingia kwenye biashara baada ya matokeo ya kidato cha nne kuja tofauti na matarajio aliyokuwa nayo. Anatushirikisha jinsi alivyoanzia kwenye biashara ya familia, kuiendesha vizuri na hatimaye kupata umiliki kamili wa biashara hiyo.

Zaidi anatushirikisha jinsi ambavyo amekuwa anajiwekea malengo ya faida kwa mwaka na kugawa kwa wiki na zoezi lake la kuweka akiba kila siku isiyopungua elfu 30.

Haya ni mahojiano muhimu kusikiliza kwa sababu kuna mengi ya kujifunza kupitia mwanamafanikio mwenzetu.

Mwisho kabisa ni mjadala wa pamoja wa wanamafanikio wote ambao wamekuwa na michango mizuri kwa kipindi kizima, kuanzia ushauri na maswali mbalimbali.

Tenga muda usikilize kipindi hiki kwa kina, ujifunze na kuchukua hatua ili kuweza kufika kwenye viwango vya juu kabisa vya mafanikio.

Kocha.



This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com