Listen

Description

Habari Mwanamafanikio?

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo tumepata nafasi ya kujadili kwa kina uchambuzi wa kitabu kinachoitwa Breakfast With Seneca.

Ni kitabu kinachoelezea vizuri falsafa ya Ustoa kwa namna inavyoweza kutumika kwenye zama tunazoishi sasa.

Mwandishi amekusanya pamoja kazi za Seneca kwa namba ambayo zinajibu changamoto nyingi tunazokabiliana nazo kwa sasa.

Baadhi ya changamoto kubwa ambazo kitabu hiki kimeziangalia ni;

* Hasira.

* Hofu na wasiwasi.

* Utajiri na Umasikini.

* Magumu na changamoto mbalimbali.

* Muda.

Kwa ujumla, kitabu kizima kinatusaidia kuweza kuishi maisha mazuri na yenye maana ambayo yana vitu vitatu vikubwa ambavyo ni;

* Uhuru kamili.

* Utulivu wa ndani.

* Furaha ya kudumu.

Mwisho kabisa mwandishi ametushirikisha mazoezi 17 ya kifalsafa ya Ustoa ya kufanya kila siku ili kuiishi falsafa hii kwa vitendo. Hayo ni mambo ambayo unaweza kuyafanya kwenye kila siku ya maisha yako na yakawa bora kabisa.

Karibu sana usikilize kipindi hiki, ili uweze kujifunza falsafa ya Ustoa kwa kina na uwe na maisha bora.

Kocha.



This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com