Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo unakwenda kujifunza mambo matatu makubwa.
Moja ni Nguvu ya fikra kwenye safari ya mafanikio. Hapa utajifunza jinsi fikra zako zilivyo na nguvu ya kuumba na jinsi ya kujenga fikra sahihi na kuzilinda.
Mbili ni uchambizi wa kitabu cha The Prophet ambapo utajifunza mambo mengi kuhusu maisha, makubwa yakiwa Upendo, Kazi na Thamani.
Tatu utajifunza kutoka kwa mwanamafanikio mwenzetu Sebastian Kalugulu kwenye safari yake ya mafanikio ambayo ina mafunzo mengi ya mapambano bila ya kukata tamaa.
Karibu sana usikiliza kipindi hiki ili uweze kujifunza na kuweka mapambano zaidi katika safari ya mafanikio.
Kocha.