Habari mwanamafanikio?
Karibu kwenye kipindi hiki cha ONGEA NA KOCHA ambapo unakwenda kujifunza yafuatayo.
Kwenye somo la juma utajifunza umuhimu wa kuwa kwenye jamii ambayo inakuwajibisha ili kuweza kufanya makubwa. Kwa asili sisi binadamu ni wavivu na huwa tunapenda kufanya vitu rahisi. Lakini hivyo haviwezi kutufikisha kwenye mafanikio. Tunahitaji sana kuwa kwenye jamii zinazotusukuma kufanya makubwa ili tuweze kufanikiwa.
Kwenye kitabu cha juma tunajifunza kutoka kitabu kinachoitwa Tribe: On Homecoming and Belonging kilichoandikwa na Sebastian Junger. Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii na hivyo tunafanya vizuri sana tunapokuwa ndani ya jamii inayotuelewa, kututegemea na kutuwajibisha pia. Nguvu ya jamii imepungua sana kwa sasa na kuwa chanzo cha changamoto nyingi ambazo watu wanapitia. Kwenye kitabu hiki utajifunza jinsi ya kurudisha nguvu ya jamii kwenye maisha yako ili uweze kupiga hatua kubwa.
Kwenye mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu tumepata nafasi ya kuongea na Wakili Isaack Zake ambaye ametushirikisha safari ya maisha yake ya mafanikio. Akieleza safari ya miaka yake kumi ya kujiajiri kama wakili na kuchagua kubobea kwenye eneo la sheria za kazi. Ametushirikisha pia makosa ambayo waajiri wengi wamekuwa wanafanya na yanawagharimu sana. Na kubwa zaidi, ameeleza jinsi ambavyo ameweza kutumia vizuri KISIMA CHA MAARIFA kuweza kupiga hatua kubwa. Haya ni mahojiano muhimu sana kusikiliza kwa sababu utajifunza kwa upande wa mafanikio na upande wa kuajiri pia.
Mwisho ni mjadala wa wanamafanikio wote ambao wameuliza maswali na kuchangia mambo mbalimbali kuhusu kipindi hiki. Kuna mengi mazuri ya kujifunza kupitia mjadala wa wanamafanikio wote.
Karibu usikilize kipindi hiki, ujifunze na kwenda kuchukua hatua ili kuweza kufanya makubwa zaidi.
Niendelee kukukumbusha kwamba KISIMA CHA MAARIFA ni jeshi, tunajenga jamii ya tofauti, yenye ushirikiano mkubwa na kuwajibishana ili kila mmoja aweze kufanya makubwa kwenye maisha yake.
Tekeleza wajibu wako kama mwanajeshi wa KISIMA, kwa kupambana kuliishi kusudi lako na kufikia ndoto zako kubwa huku ukishirikiana kwa karibu na wanamafanikio wenzako kupitia klabu za KISIMA CHA MAARIFA.
Kocha.