Wakenya wamekuwa wakiskia habari za kufedhehesha kumhusu Seneta wa Lamu; mara amefyatua risasi, mara amefyatuliwa risasi, mara binti amedai kupigwa naye. Visa hivi vingi vinaripotiwa kufanyika usiku wa manane. Tunautaja huo kuwa ukiukaji wa sura ya katiba inayohusu uongozi na maadili.